The United Republic of Tanzania

Tume ya TEHAMA kujenga maabara ya kwanza ya vifaa vya kieletroniki ndani ya TIRDO

Tume ya TEHAMA kujenga maabara ya kwanza ya vifaa vya kieletroniki ndani ya TIRDO

TUME ya Tehama nchini (ICTC) na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) zimesaini Mkataba wa Maelewano (MoU) kwa ajili ya kujenga Maabara ya Kutengeneza, Kukarabati na
Kuunganisha Vifaa vya Kieletroniki nchini.

Maabara hiyo ya kisasa ambayo inatarajiwa kujengwa na tume ndani ya shirika hilo inatarajiwa kuwa fursa kubwa kwa vijana kustawisha bunifu zao nchini.

Pia, taasisi hizo za umma zitashirikiana katika sekta zingine kama kuunganisha vifaa vya kielektoniki, kufanya matengezo vifaa vilivyoharibika. Vile vile kutoa mafunzo ya kitalam kwa wataalam wa TEHAMA na kuhuisha vifaa vilivyokwisha muda wake ili viweze kuingia sokoni tena kwa matumizi.

Read more
Hongerenii sana Tume ya TEHAMA

Hongerenii sana Tume ya TEHAMA

Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga kwa niaba ya watoa mada kuu walioshiriki katika Kongamano la Nne la Kitaaluma la Biashara na Uchumi lililofanyika jana jijini Dodoma chini ya uratibu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE). Dkt. Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo, alikabidhi vyeti kwa kutambua mchango wa wazungumzaji hao kwenye tasnia ya Taaluma, Biashara na Uchumi na kipekee, aliishukuru Tume ya Tehama kwa kutekeleza vyema majukumu yake tangu ilipoasisiwa katika Serikali ya Awamu ya Nne. (Mpiga Picha Wetu).

Read more